Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) , Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema chama hicho hakikurupuki katika kuwekea malengo ya serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Amesema CCM imekuwa ikiilekeza serikali kutekeleza shughuli za maendeleo kupitia ilani ya uchaguzi yenye mambo yote , ikiwamo miradi mbalimbali kama vile afya ,maji elimu na miondombinu .

Amesema hayo kwenye mkutano wa kampeni, uliofanyika wilayani longido mkoani Arusha wakati akimuombea kura Rais John Magufuli pamoja na mgombea ubungo jimbo la Longido ,Dokta Stephen Kiruswa.

Katika hatua nyingine Majaliwa amesema kuwa serikali itaenndelea kuimarisha sekta ya mifugo ili kukuza uchumi wa nchi na wafugaji kwa kuanzisha viwanda kikubwa cha kuchakata bidhaa za mifugo .

Alisema kuwa kiwandda hicho kina uwezo wa kuchakata n’gombe 300 hadi 500 kwa siku ,mbuzi na kondoo 3,000 hadi 4,000 kwa siku.

Mkutano huo uliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa CCM wa mkoa wa Arusha na wilaya Logindo pamoja na wagombea wa majimbo yote ya mkoa wa Arusha na wagombea wa kata  18 za wilaya ya Longido.

CHADEMA, TBC mambo safi
Ubwabwa wa Rungwe wapigwa 'Stop'