Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassimu Majaliwa amezindua wakala wa barabara za vijijni (TARURA) ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo eneo husika.

Majaliwa mezindua wakala huo mapema hii leo mjini Dodoma,ambapo amesema kuwa utakuwa ni ukombozi wa wananchi wa vijijini kusafiri na kusafirisha bidhaa zao ambazo zitakuwa ni chanzo cha kukuza uchumi wa taifa.

“Wakala huu tunaouzindua leo utakuwa na ustawi mkubwa katika nchi yetu kwa kuongeza chachu ya uzalishaji katika maeneo ya vijijini kutokana na urahisi wa usafirishaji wa bidhaa kufika sokoni,ambao utashusha bei za bidhaa mjini na kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi,”amesema Majaliwa.

Aidha, ametaja manufaa mengine ya wakala huo kuwa ni kuboresha na kubadilisha hali ya kimaisha na uchumi kwa wananchi kwani watakuwa wanasafirisha bidhaa zao kwa muda mfupi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa Manispaa zinakabiliwa na changamoto kubwa ya kuboresha miundo mbinu ya ukarabati wa barabara  zikiwemo rushwa katika utoaji zabuni.

Magazeti ya Tanzania leo Julai 3, 2017
Aliyekuwa Waziri Mkuu Israel, Olmert aachiliwa huru kutoka gerezani