Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike na ndio maana inasisitiza waachwe wasome hadi wamalize kidato cha sita.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Ruangwa ambapo anaendelea na ziara yake jimboni kwake kuhimiza maendeleo akiwa kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka.

“Tumesema mtoto wa kike aachwe asome hadi kidato cha sita, akifikia chuo kikuu atakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yake lakini kwa sasa acheni wasome, Ninyi vijana mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake miaka thelathini jela”amesema Majaliwa.

Aidha, amesema kuwa nia ya Serikali ni kupata wataalamu wa kada tofauti tofauti kama Madaktari, Wanasheria,Mafundi,Waalimu na hata wakuu wa wilaya wanawake.

DC Lyaniva awataka wakazi wa temeke kuwajibika
Video: Sakata la Watanzania Malawi laibua mapya, Makubwa yafichuka Faru John...