Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.5 kwa vikundi vya vijana 129 katika Halmashauri mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo alipokuwa akitoa hotuba yake kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato  na matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.

“Serikali inaendelea na azma yake ya kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu”’ Amesema Majaliwa.

Aidha , Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia mapato yake ya ndani zimetoa Shillingi Billioni 4.6 ikiwa ni mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi vya vijana 2,356 na hatua hizi zimekwenda sanjari na utengenezaji wa maeneo maalum yenye jumla ya ekari 85,603 kwa ajili ya shughuli za vijana za Kilimo, biashara ndogo ndogo, burudani na michezo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa katika mwaka 2017/2018, Serikali itaendelea kusimamia Halmashauri zote nchini kutenga asilmia 5 ya mapato yao kwa ajili ya vijana na asilimia 5 kwa wanawake.

Yakubu Aiyegbeni Ashindwa Kutimiza Lengo
Marufuku Kwenda Mahakamani Zanzibar