Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Tanzania imepata mafanikio makubwa kutokana na kushiriki kwake katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Amesema kuwa kikao hicho kimekuwa na tija kwa Tanzania kutokana na maeneo ya vipaumbele yaliyojadiliwa katika mkutano huo hususani masuala ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda.

Ameyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi China ambako alikwenda kumuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano wa FOCAC.

Amesema kuwa kipaumbele katika mkutano huo ni masuala ya usalama wa nchi, maendeleo ya kiuchumi hususani uboreshaji wa sekta ya viwanda, elimu, kilimo, afya, elimu na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

“Kikao hiki kimekuwa na tija kwa Tanzania kwa sababu maeneo yote yaliyojadiliwa ni muhimu kwetu. Tumeanza kuona idadi nzuri ya wawekezaji kutoka China na ni matokeo ya mpango uliowekwa katika kikao cha kwanza cha FOCAC kilichofanyika Afrika Kusini.”amesema Majaliwa

Aidha, Majaliwa amesema maeneo mengine yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na sekta ya madini, mifugo na uvuvi, ambazo nazo zimewekewa mikakati ya namna ya kuziboresha ili ili ziweze kuchangia ukuzaji wa uchumi katika mataifa hayo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kikao hiko pia kilijadili namna ya kuboresha sekta ya utalii kwa kuvutia watalii kutoka za Afrika na nje ya bara hilo ikiwemo na China, hivyo Tanzania inatakiwa kutumia fursa fursa zilizopo kuvutia watalii kutoka nchi mbalimbali.

 

 

Kwesi Nyantakyi ongezewa muda wa adhabu
LIVE: Rais Magufuli akihutubia wananchi wa Butiama