Serikali imetangaza adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu yeyote atakaye katisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzito au hata ukikutwa naye nyumbani kwako au katika nyumba za wageni.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa wilaya ya Masasi, Mtwara ikiwa ni siku ya nne ya Ziara yake ya kikazi mkoani humo.

”Tukikukuta na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria, Ole wenu vijana. mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela”. Amesema Majaliwa.

Pia ameongezea kuwa kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto wa kike ambao bado ni wanafunzi wazazi na watakaomsindikiza kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha Majaliwa amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao na wasikubali kutumika kimapenzi.

 

 

Watuhumiwa 10 chini ya ulinzi kufuatia Diwani aliyeuawa kwa mapanga
Waziri Mkuu achunguzwa kesi ya uhujumu uchumi