Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa watu wote watakaothibitika kufanya vitendo vya kukatisha watoto wa kike ndoto za kuendelea na masomo ikiwemo miaka 30 jela.

Ametoa kauli hiyo wakati akiweka Jiwe la Msingi na kukabidhiwa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Bunge High School iliyojengwa na Wabunge katika Kata ya Kikombo jijini Dodoma kwa thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni moja.

Mbunge Bungara (Bwege) atimkia ACT Wazalendo

”nyie vijana mtoto wa kike aachwe aende kusoma ukimfuatafuata miaka 30 itakuwa inawasubiri, nawaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya kijiji na kata msimamie utekelezaji wa sheria hii ili kumlinda mtoto wa kike” amesema Waziri mkuu Majaliwa

Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote nchini wahakikishe wanaendelea kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama hadi ngazi za kata kusimamia Sheria ya Elimu ya kuwalinda watoto wote wa kike walio chini ya umri wa miaka 18.

Sera za Nyalandu na Mchungaji Msingwa Wanavyoutaka Urais 2020

Serikali yapiga marufuku Mgonjwa kudaiwa damu kabla ya huduma

Balozi Karume ajitosa Urais Zanzibar (CCM)
Polisi aliyemuua Mmarekani mweusi kwa risasi kushtakiwa