Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania kushirikiana na kushikamana ili kuyapa thamani madini ya Tanzanite na kuifanya dunia nzima itambue kuwa madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya sita tayari imeweka mazingira ya kuyaongezea thamani madini hayo.
 
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo Januari 26, 2022 alipozungumza na wananchi katika eneo la EPZA unapojengwa Mji wa Tanzanie katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Manyara.
 
Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha rasilimali zote zilizoko nchini yakiwemo madini ya Tanzanite zinawanufaisha wananchi wote hususani wanaoishi katika maeneo zinapopatikana.
 
Amesema kuwa Serikali itaendelea kukutana na wafanyabiashara wa sekta madini kwa lengo la kuhakikisha kwa pamoja wanaweka mikakati ya kusaidia kuikuza sekta hiyo ili iendelee kuleta tija kwa watanzania na taifa kwa ujumla.
 
Akizungumza baada ya kukagua eneo la uwekezaji la EPZA, Waziri Mkuu amewataka watanzania kujitokeza na kuwekeza katika eneo hilo “Watanzania tumieni fursa ya eneo hili kuwekeza mtakapa faida”
 
Hata hivyo Waziri Mkuu Majaliwa amewahimiza wananchi waendelee kufanya biashara hiyo ambayo ina manufaa makubwa kwao na Taifa kwa ujumla na kwamba Serikali ipo tayari kuwahudumia wakati wote.

Simba SC yabamizwa Kagera
Wakandarasi wapewa wiki mbili