Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Dar es Salaam hadi Kilosa mkoani Morogoro na kusema ameridhika na hatua iliyofikiwa.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo septemba 12 katika kituo cha Kwala kilichopo mkoani Pwani ambacho kitatumika kama kituo kikuu cha kufanya matengenezo makubwa ya mabehewa na injini za treni.

Waziri Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu amedhamiria kukamilisha ujenzi wa miradi yote iliyoanzishwa hivyo kuwataka watanzania kuwa na imani na serikali yao na ameahidi kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati uliopangwa awali.

Aidha Waziri Mkuu amewasihi wafanyakazi wa mradi huo kufanya kazi kwa ufanisi kwani lengo la serikali ni kufikisha mradi huo katika mikoa ya Mwanza, Kigoma, na Katavi katika bandari ya Kalema.

Ujenzi wa reli ya kisasa itawezesha kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kwa kuwa Tanzania ni nchi ya kimkakati na nchi zote jirani zinategemea reli hiyo.

Hamid Mir: Simulizi ya mwandishi wa Pakistan aliyemhoji Osama bin Laden mara tatu
Naibu Waziri Ummy : Akemea ukatili kwa vijana