Hospitali ya Muhimbili imeingia tena katika matatizo ya kutokuwa na huduma za upimaji wa kutumia mashine za Magnetic Reasonance Imaging (MRI) baada ya mashine hizo kuharibika tena siku mbili baada kutengenezwa kufuatia agizo la Rais John Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo.

Mashine hiyo ilitengenezwa na Kampuni ya Phillips na kuanza kufanya kazi huku ikianza kwa kumhudumia mgonjwa aliyeomba msaada wa Rais Magufuli alipoitembelea hospitali hiyo.

Mbali na mashine hiyo, bado matengenezo ya mashine ya CT-Scan hayajafanikiwa hivyo wagonjwa watarejea hali yao ya zamani ya kutafuta vipimo hivyo kwenye hospitali binafsi.

“Mapema wiki iliyopita tuliwatangazia wananchi kwamba huduma ya MRI zimeanza kutolewa baada ya mashine hiyo kutengenezwa. Katika taarifa hiyo tuliwaeleza kuwa matengenezo ya kifaa kingine cha CT-Scan yalikuwa yakiendelea,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha.

“Hata hivyo baada ya mashine ya MRI kufanya kazi Novemba 11 na 12, mwaka huu iliyoonekana kuwa na hitilafu ya kiufundi ambayo inahitaji matengenezo zaidi, hali ilyotulazimu kusimamisha kufanya kazi kuanzia Novemba 13 mchana,” Aligesha aliongeza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

 

Donald Trump ‘Achafua Hewa' Tena Na Hili Kuhusu Misikiti ya Marekani!
Ndugai: Tutegemee Migomo Bunge La Kumi Na Moja, Kupambana na Ole Medeye