Mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi nchini iliyoahidiwa na Rais John Magufuli iko katika hatua za mwisho kukamilika ambapo majaji 14 wamepangwa kufanyiwa mafunzo maalum ya uendeshaji wa kesi hizo.

Akizungumza jana baada ya kutembelea mabanda ya Mahakama Kuu katika maadhimisho ya wiki ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu, Othman Chande alisema kuwa majaji hao 14 watanolewa katika chuo cha Sheria cha Lushoto.

Alisema kesi zote ambazo ushahidi wake utakuwa umekamilika, zitasikilizwa ndani ya kipindi cha miezi 9.

“Zile kesi ambazo ushahidi uakuwa umekamilika hatutaki zidumu mahakamani kwa zaidi ya miezi 9. Hizi ni jitihada ambazo tunafanya hata kwa mahakama nyingine kwa sababu tumepokea maoni ya wananchi wanasema wanakera na ucheleweshwaji wa kesi na wengi wanasema bora kesi iwahishwe kuliko kuamriwa sawa,” Jaji Mkuu anakaririwa.

Jaji Chande alisema kuwa baada ya Bunge kupitisha marekebisho ya sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 ya mwaka 2002, marekebisho yaliyoanzisha mahakama hiyo, wako katika mchakato wa kuandaa kanuni za sheria zitakazotoa nafasi ya kufungua masijala yake pamoja na kuwalinda mashahidi wa kesi hizo.

Majengo ya mahakama ya Mafisadi itajengwa pembeni ya shule ya sheria (law school), iliyoko Sinza jijini Dar es Salaam.

 

 

Picha: Diamond afanya mazungumzo haya na Waziri Mkuu nyumbani kwake
UVCCM waionya BAVICHA, wadai watapambana kama ‘MauMau’