Waombolezaji takribani 380 wamenusurika kifo baada ya kugundua kutumia maji ya kisima yenye sumu kwa kupikia na kunywa mara baada ya mifugo wakiwemo ng’ombe 16 kufa papo hapo baada ya kunywa maji hayo.

Mifugo mingine iliyokufa kwa kunywa maji hayo ni punda, bata na paka. Tukio hilo limeripitiwa kutokea juzi katika kijiji cha Mkusa katika bonde la ziwa Rukwa wilaya ya Sumbawanga na kusababisha taharuki kwa waombolezaji waliokusanyika kwenye nyumba ya ya mfugaji Elias Juma.

Taarifa kutoa eneo la tukio zinaeleza kuwa kabla ya waombolezaji hao hawajaanza kuyatumia maji yaliyokuwa kwenye kisima cha Juma, wanyama walichotewa na walipoyanywa walikufa papohapo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watu wawili wamekamatwa na wanashikiliwa na jeshi la polisi wakituhumiwa kumwaga sumu katika kisima.

Ameeleza kuwa wawili hao ni majirani wa mfuaji Juma ambapo walishtakiana mahakamani katika shauri la mgogoro wa aridhi.

“Maofisa polisi na mtaalamu wa afya walifika kijijini hapo na kufanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kuwa mifugo hiyo ilikunywa maji yenye sumu ambayo haikuweza kufahamika mara moja ” Ameeleza kamanda Masejo.

Amethibitisha kuwa hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kupoteza maisha kutokana na tukio hilo, na kubainisha wanayama waliokufa ni ng’ombe wa kisasa 16, punda, bata pamoja na paka.

Luc Eymael auponda uwanja wa Karume
Tshishimbi awasihi Mashabiki/Wanachama