Leo Februari mosi Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amejibu swali la Mbunge wa viti maalumu (Chadema) , Suzan Lyimo  kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu matumizi ya sindano za kuongeza maumbile ambazo zina madhara kwa mwili wa binadamu.

Ndugulile amejibu amesema kuwa sindano hizo zina madhara makubwa mwilini, Serikali hairuhusu jambo hilo, dawa zote ambazo hazijasajiliwa zinapigwa vita  kwa kuwa zina madhara kwa watumiaji.

Ameongezea kuwa mwili wa binadamu umeumbwa kwa namna ya asili kwa lengo la kujikinga na mambo mengi ikiwemo mionzi.

Suzan ameibua hoja hiyo bungeni pindi alipokuwa akiuliza swali la nyongeza na kubainisha kuwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wanawake kutumia sindano hizo, kama Serikali inalijua jambo hilo imechukua hatua gani.

“Naomba kujua iwapo serikali ina taarifa kwamba wapo wanawake wanaotumia sindano kwa ajili ya kuongeza maumbile yao, kama wanapata madhara  Serikali imechukua jukumu gani kukomesha jambo hilo,” amesema Lyimo.

 

Mahakama yaingilia kati agizo la Kenyatta kuzimwa kwa vyombo vya habari
Video: Uhamiaji yaelezea faida za Hati za kusafiria za 'Kielektroniki'