Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus, wametangaza kusaini mkataba mpya na mabeki wakongwe Giorgio Chielini na Andrea Barzagli.

Chiellini mwenye umri wa miaka 33, ambaye ametangazwa kuwa nahodha mpya wa The Bianconeri, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili ambao utamfikisha mwaka 2020, huku mkongwe mwenzake Barzagli mwenye umri wa miaka 37, akisaini mkataba wa mwaka mmoja ambao utamuwezesha kuwepo Juventus hadi 2019.

Wawili hao ni miongoni mwa wachezaji watano waliofanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya Italia mara saba mfululizo, jambo ambalo limewapa heshima na kuonekana bado wana uwezo wa kuisaidia klabu hiyo, ili ifikie malengo kama hayo kwa mara ya nane msimu wa 2018/19.

Uongozi wa Juventus umeridhishwa na majibu ya tathmini iliyofanywa pindi wawili hao wanapocheza kwa pamoja uwanjani, ambapo imebainika kuwa, msimu uliopita waliruhusu kufungwa asilimia 0.7 na kuisababishia timu asilimia 2.3 za pointi walizozipata.

Pia tathmini hiyo imebaini wawili hao walipowekwa pembeni na nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji wengine timu ilikubali kufungwa kwa asilimi 0.8 na kupata asilimia 2.2 za point kwa kila mchezo.

Mpaka sasa Chiellini ameshaitumikia Juventus katika michezo 472, na amekua mchezaji wa saba kucheza kwa muda mrefu klabuni hapo katika historia ya klabu hiyo ya mjini Turin.

Kwa upande wa Barzagli amecheza michezo 199 tangu alipojiunga na Juventus mwaka 2011 akitokea Vfl Wolfsburg.

Marcelo Vieira da Silva Júnior aumiza vichwa madaktari
Ki Sung-yueng arudi ligi kuu England