Kalimangonga Ongala amerejea tena kwenye klabu ya Majimaji ya mjini Songea baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Young Africans ambaye msimu uliopita aliifundisha timu hiyo na kuinusuru kushuka daraja, anatarajiwa kuanza mara moja majukumu yake ili kuinusu timu hiyo ambayo mpaka sasa haijashinda mchezo hata mmoja baada ya kucheza michezo sita.

Ongala, ambaye ni mtoto wa marehemu Remmy Ramdhani Mtolo Ongala, pia ameshawahi kuwa kocha msaidizi wa Azam FC chini ya Marius Omog kabla ya kutimuliwa misimu kadhaa iliyopita.

Ikumbukwe katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita, Majimaji ilipokea kipigo kikubwa cha mabao 4-0 kutoka kwa Simba, mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Jurgen Klopp: Nampenda Sana David Silva
Lipumba akomaa na Lowassa, ‘nilisoma naye…’