Wamiliki na mameneja wa hotel na nyumba zote za kulala wageni nchini Uganda, Kampala wametakiwa kusalimisha majina ya wageni wote wanaokuja kulala kwenye sehemu hizo katika kituo chochote cha polisi kilichopo jirani nao.

Polisi Uganda wametoa sera hiyo mpya ambayo inawalazimisha wamiliki na mameneja wa Hoteli, nyumba za kulala wageni na maeneo mengine kusalimisha majina hayo polisi.

Afisa Mwandamizi wa Polisi , Asan Kasingye amesema kuwa wameamua kufuatilia suala hilo kwa nyumba zote za biashara za kulala wageni kwa lengo la kuimarisha ulinzi jijini hapo na maeneo jirani.

Kasingye ameongezea kuwa majina hayo yatakayowasilishwa yatakuwa yanatumika na maafisa usalama kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za wageni wanaotembelea maeneo hayo, kufahamu maeneo wanayotoka na wanakoelekea.

Ambapo orodha hiyo ya majina itatakiwa kupelekwa Kituo cha Polisi mapema asubuhi.

Kabla ya sera hiyo wamiliki wa nyumba pekee ndio walikuwa wanalazimishwa kupeleka orodha ya wapangaji wao kwa viongozi wa mitaa na kisha nakala kupelekwa Polisi.

AfDB kuipa Tanzania zaidi ya Sh 1 trilioni kujenga uwanja wa ndege Dodoma
TANESCO yatakiwa kuondoa vikwazo

Comments

comments