Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini, Amri Athman maarufu kama Majuto ameomba kusaidiwa kumjua mtu ambaye kipindi akiwa mgonjwa anamzushia kifo na hii ikiwa mara ya nne.

Mapema leo hii kumekuwa na uvumi wa taarifa iliyodai kuwa Mzee Majuto amefariki dunia taarifa ambayo imeshtua wengi.

Mzee Majuto ana masaa 12 tangu aruhusiwe kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akiendelea kupata matibabu ya ugonjwa uliokuwa unaomsumbua mara baada ya kurejea nchini India mnamo Juni 22, 2018.

”Mimi ni mzima niko nyumbani kwangu, nimeshatoka hospitali ya Muhimbili nilipokuwa nimepumzishwa, sijafa huyo aliyenizushia taarifa hizo namuomba tu anionee huruma kwa sasa maana hii adhabu niliyonayo ya kuumwa inatosha, japo kuumwa ni ibada kama nimekosea anisamehe kwani hii sio mara ya kwanza kuzushiwa kifo ni zaidi ya mara nane, sijui nimemkosea nini amehoji Mzee Majuto.

Ameongezea kuwa ”Kitu ambacho sijakielewa hadi sasa ni pale mimi kuzushiwa kifo hasa nikiwa mgonjwa, mtu anapigilia msumari hapohapo, Ni kitu kibaya sana kumzushia mwenzio kifo na naona roho yangu anaitaka muda mrefu, naombeni kunisaidia kujua ni nani huwa anaanzisha hizi habari”.

Aidha Chama cha Waigizaji nchini TFDAA, kimetoa onyo kali kwa mtu yeyote atakayeshikwa kusambaza habari hizo za uzushi na kimeahidi kumuwajibisha kisheria.

 

Ndugai: Endapo mtaikataa bajeti ya Serikali, Rais atalivunja bunge
Video: Wabunge waamsha 'dude' la korosho, Wabunge CCM wagawanyika