Jamii imetakiwa kufahamu kuwa Kamati za Mazingira katika ngazi zote zipo kwa mujibu wa sheria, sheria ya Mazingira kifungu Na. 38 (1-2) na Kamati hizo zina wajibu wa kusimamia mazingira kikamilifu yanayohusu maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba alipokuwa akizungumza na Watendaji wa Mkoa wa Tabora katika hafla ya kuzindua Kamati ya Usimamizi wa mazingira Mkoani humo.

Amesema kuwa uanzishwaji wa Kamati za Mazingira katika ngazi za vitongoji, vijiji na kata nchi nzima na kuahidi kutuma wataalamu kutoa mafunzo kwa kamati hizo.

“Naagiza kila Halmashauri kufahamu kiwango cha uzalishaji wa taka, hii itasaidia kuja na miradi ya kuzalisha nishati mbadala pale fursa zitakapopatikana. Ukiazima kitu kwa mtu yeyote huna budi kukitunza na kukulinda ila kukirudisha kwa mwenyewe kikiwa katika hali nzuri.” amsema Makamba

Aidha, Makamba ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Tabora kuteua ama kuajiri Maafisa wa mazingira wa kutosha ili kusimamia kikamilifu uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira, pamoja na kuandaa mpango tekelezi wa mazingira katika ngazi ya Mkoa.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amemueleza Waziri Makamba jinsi Mkoa wake unavyotekeleza kikamilifu kampeni ya upandaji miti kwa kuwa na kauli mbiu ya ‘Tabora ya Kijani’ na  amemshukuru kufanya ziara katika Mkoa huo.

 

Utafiti: Njugu zinavyoboresha nguvu za kiume
Video: Utata kesi ya kina Mbowe, Bunge lanusa harufu ya ufisadi