Waziri wa Nishati, January Makamba ameahidi kufunga mtambo wa Gesi wa Tani moja (Kilogram 1,000), kwenye Chuo cha Ukunga na Uuguzi cha Peramiho Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma ili kiwe cha mfano.

Makamba ametoa ahadi hiyo baada ya kukagua mfumo wanaotumia kupikia kwa kutumia magome ya miti na kusema Serikali itafanya tathmini kabla ya kufungwa kwa mtambo huo na kuanza kutoa ruzuku kwa Taasisi kama hizo zitakazofunga mifumo ya Gesi ya kupikia.kutafanyika

Akiwa katika ukaguzi wa mfumo huo wa kupikia, Waziri Mkamba pia alijionea changamoto mbalimbali zinazolikabili eneo hilo, ikiwemo kutoa moshi mwingi na kusababisha Wanafunzi zaidi ya 170 kuchelewa kupata chakula.

Amesema, “kama mnavyofahamu, tunatoa mitungi ya Gesi kwa makundi mbalimbali vijijini lakini pia kufunga mifumo ya kupikia ya gesi katika taasisi mbalimbali, lengo letu ni kuwaondelea wananchi adha ya kupika kwa kutumia kuni na mkaa, na huu ni utekelezaji wa Sera ya Nishati ya mwaka 2015.”

Aidha, amesema kufungwa kwa mifumo ya gesi katika chuo hiki kutawezesha Serikali kupata taarifa sahihi na kujifunza jinsi Taasisi zinavyoweza kumudu na kutumia mifumo hiyo ya kupikia na kwamba shule hiyo itakuwa ni mfano wa mabadiliko kutoka nishati chafu kwenda nishati safi ya kupikia.

Awali, Mkuu wa Chuo Uuguzi cha Peramiho, Sista Evodia Ngonyani alimshukuru Waziri Makamba kwa kutembelea chuoni hapo na kuona jinsi wanavyopika katika mazingira ambayo si salama, kutokana na wapishi muda wote kuwa katika mazingira ya moshi ambayo ni hatari kwa afya na katika mfumo wa upumuaji.

Shule hiyo, itafungiwa mfumo wa kupikia ambao utajumuisha mtungi wa gesi wa tani moja, mabomba na mfumo wa kupikia  wenye majiko makubwa matatu na sufuria zake za kupikia kubwa zenye uwezo wa kuhudumia watu 200.

Ne-Yo aomba faragha tuhuma za usaliti na Machangudoa
Haji Manara amuangukia Waziri Mchengerwa