Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba, amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Nchini (National Environmental Trust Fund – NETFUND).

Makamba amefanya uteuzi huo mapema hii leo jijini Dar es salaam kufuatia uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua Ali Mafuruki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini  wa Mfuko  huo.

Aidha, Makamba amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Sheria ya mazingira Sura ya 191 ya mwaka 2004, kifungu cha 215 (2).

Amewataja wajumbe walioteuliwa kuwa ni Mwajuma Mbogoyo, Emelda Teikwa, Profesa Razak Bakari Lokina na  Hatibu Senkoro.

Wengine ni Alesia Mbuya, Baraka Juma Kalangahe,Dkt. Andrew Komba na Profesa Yunus Mgaya.

Hata hivyo, Makamba amesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja na kuwatakia kila la heri wajumbe wapya wa Bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa katika Sheria.

Maelfu yamiminika kulipa deni Bodi ya Mikopo, picha za wadaiwa kuanikwa
Kamati ya bunge la Marekani yaanza uchunguzi dhidi ya Urusi