Serikali nchini, imeamua kutekeleza mradi wa Umeme wa Maji ya Rumakali uliosanifiwa tangu mwaka 1998 Wilayani Makete Mkoa wa Njombe, ili kuwezesha nchi kuwa na Umeme wa kutosha toka kwenye vyanzo mbalimbali vya Nishati.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati akiwa Wilayani Makete Mkoa wa Njombe kwenye ziara yake ya kikazi ya Kijiji kwa Kijiji, inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini, ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi juu ya changamoto za Nishati ya umeme.

Waziri Makamba, akiwa katika mradi wa kufua umeme kwa Njia ya Maji wa Rumakali (MW 222), wenye thamani ya Shilingi 1.4 Trilioni uliosanifiwa tangu mwaka 1998 amesema, Serikali imeamua kutekeleza mradi huo wa Umeme wa Maji ya Rumakali ili kuwezesha nchi kuwa na Umeme wa uhakika.

Amesema, “Serikali imeamua kutekeleza mradi wa Umeme wa Maji ya Rumakali uliopo Wilayani Makete Mkoa wa Njombe ili kuwezesha nchi kuwa na Umeme wa kutosha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya Nishati.”

Hata hivyo, amefafanua kuwa kuanzia Agosti 1, 2022, wathamini watafika eneo hilo ili kuzungumza na Wananchi juu ya maeneo yatakayochukuliwa na Serikali, ili kuanziasha mchakato wa fidia kwenye eneo hilo la Kilometa za Mraba 13.2 za mradi.

Awali, wakiongea mbele ya Waziri Makamba Wananchi hao wamesema, walishakata tamaa ya kuendelezwa kwa mradi huo, na kwamba kwasasa wamepata matumaini huku wakiamini utatekelezwa kwa vitendo.

Afariki nyumba ya wageni, mpenzi wake ashikiliwa na Polisi
Mtandao wa Wanawake wavuvi wazinduliwa