Waziri wa Nishati, January Makamba, amefanya mazungumzo na viongozi wakuu wa kampuni ya Shell iliyopo nchini Uholanzi, kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa mradi wa LNG nchini Tanzania.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Makamba alielezea azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mazungumzo yanakamilika, ili baada ya Disemba mwaka huu hatua za utekelezaji ziweze kuanza.

Amesema, “Mpango wa Serikali wa kuanzisha Ofisi Maalum ya Kusimamia Utekelezaji wa Mradi wa LNG (Tanzania LNG Office) mnamo mwezi Novemba mwaka huu kwa lengo la kuratibu, kuharakisha na kurahisisha hatua za utekelezaji wa mradi.”

Mazungumzo Kati ya Waziri Makamba na viongozi wakuu wa kampuni ya Shell iliyopo nchini Uholanzi, kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa mradi wa LNG nchini Tanzania.

Mradi huo, wa kuchakata na kusindika gesi asilia iliyogundulika katika bahari kusini mwa Tanzania, utafanikisha uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 40 nchini, na unatekelezwa na Makampuni ya Shell ya Uholanzi, Equinor ya Norway na washirika wao.

Hata hivy, Waziri Makamba ameongeza kuwa, mradi huo una manufaa mengi kwa Tanzania na utafungua fursa kwa wananchi wa Mikoa ya Kusini mwa Tanzania ikiwemo kuongezea mapato ya nchi, kuleta ajira, mapinduzi ya kiuchumi na kijamii nchini.

Akiongea katika mazungumzo hayo, mwakilishi kutoka Shell, John Crocker, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapa wawekezaji matumaini na kutoa kipaumbele katika mradi huo uliosainiwa kwa mkataba wa awali.

Amesema, ameridhishwa na hatua ya majadiliano iliyofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo na kusisitiza nia yao na ya washirika ya kutekeleza mradi huo.

Mazungumzo hayo yamefanyika chini ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba kwa kuwahusisha Makamu wa Rais anayeshughulikia miradi ya LNG, Cederic Cremers na Makamu Rais wa Shell, John Crocker anayehusika na Mahusiano ya Serikali.

Taarifa binafsi za mitandao ya simu kulindwa
Mataifa yakumbushwa kuepuka uchafuzi hali ya hewa