Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amemsimamisha mwanasheria wa Baraza la Mazingira Nchini (NEMC), Heche Suguta, aliyekuwa msimamizi wa zoezi la bomoabomoa.

Suguta amesimamishwa kazi baada ya kubainika kuwa amekiuka miiko ya kazi katika kusimamia kiwanda cha kusindika minofu ya punda kilichoko mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamo wa Rais, Waziri Makamba alichukua hatua hiyo kufuatia kikao cha ndani kilichofanyika juzi kikilenga kujadili na kuimarisha utendaji wa NEMC.

Pamoja na Suguta, watumishi wengine wawili waliosimamishwa kazi kwa kukiuka miiko ya kazi ni Afisa Mazingira Mwandamizi, Dk. Eladius Makene na Afisa Mazingira, Boniface Kyaruzi.

Idris na wema wanatarajia mtoto, idris amuandika ujumbe mtamu akimuita 'wife'
Vijana wa CCM wamvaa Membe, wamtaka amuache Magufuli