Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amewataka wachimbaji mchanga na walima bustani katika bonde la mto msimbazi katika kata vingunguti iliyopo Manispaa ya Ilala, kuondoka mara moja na kuacha shughuli hizo.

Ameyasema hayo alipokua katika ziara ya siku moja ya kutembelea kata ya Vingunguti na kujionea athari mbalimbali za kimazingira katika kata hiyo.

Aidha, wakiongea mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamelalamikia kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo bonde hilo kuzidi kumong’onyoka na kusogelea makazi ya watu pamoja na eneo la makaburi. hivyo kusababisha nyumba zao kuanguka na makaburi kumong’onyoka hali amabayo inahatarisha maisha yao na kuwafanya kuishi kwa hofu.

Hata hivyo, akijibu kero hiyo Waziri Makamba amesema kuwa atayafanyia kazi maombi yao na atakaa na viongozi wa Manispaa na wa Ofisi yake ili kupata suluhu ya matatizo yao. Pamoja na hayo amesema kuwa kwa hatua za awali amewataka  wachimbaji na wakulima wa bustani kuacha mara moja shughuli hizo wanazofanya katika maeneno ya bonde hilo.

Samia suluhu asisitiza ushirikiano bonde la mto Nile
Ventura Apuuza Utayari Wa Federico Fazio