Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, January Makamba leo amelitangaza eneo la Mbeya Mountain Range kuwa eneo nyeti la mazingira kutokana na unyeti wake kwa mazingira ya jiji hilo.

Makamba ambaye anaendelea na ziara yake mikoani, amechukua uamuzi huo mkoani Mbeya kwa mujibu wa   Kifungu cha 51 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 inayompa waziri mwenye dhamana mamlaka ya kutangaza eneo lolote kuwa nyeti.

“Nimefanya maamuzi haya kwasababu vyanzo vya maji yanayokuja Mbeya yanatokea huko lakini watu wameshindwa kabisa kudhibiti uharibifu wa vyanzo hivyo. Miaka ya nyuma kulikuwa na vyanzo 49 lakini sasa vimebakia vinne tu,” alisema.

makamba-2

Ameongeza kuwa amri hiyo itatangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali (Government Gazette) wiki ijayo ili usimamizi wake uanze rasmi.

Waziri huyo mwenye dhamana ya usimamizi wa mazingira alifafanua kuwa tangazo hilo litaweka zuio la kisheria la matumizi ya kibinadamu katika milima hiyo, ikiwemo uvunaji wa miti unaofanywa na Mamlaka ya Misitu Tanzania (TFS). Pia, aliagiza milima hiyo kuanza kupandwa miti ya asili inayohifadhi maji.

makamba-4

Mji wa Mbeya kwa sasa unahitaji lita milioni 50 za maji kwa siku, kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji katika safu ya milima ya Mbeya, ifikapo mwaka 2018 maji katika mji huo hayatawatosha wakaazi wake.

Waziri Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli alisema kuwa ingawa hii ni mara ya kwanza kifungu hicho cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, kuna nia ya kutangaza maeneo mengi zaidi.

Harakati Za Kupanda Ligi Kuu Kuendelea Wikiendi Hii
Kampuni ya TANMAT yatozwa faini ya sh. mil.50 kwa uchafuzi wa mazingira