Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba amesema kuwa changamoto za Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka 15 mwaka 2006 hadi kufikia changamoto 3 mwaka 2017.

Ameyasema hayo mapema hii leo Mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati nchi ikielekea katika maadhimisho ya Muungano unaotimiza miaka 53 wiki ijayo.

Amesema kuwa  changamoto zilizobakia kuwa ni pamoja na usajili wa vyombo vya moto unaorahisisha kusafirisha magari kutoka Zanzibar kwenda Bara na kutoka Bara kwenda Zanzibar na kuongeza kuwa kero hiyo inafanyiwa kazi kwa kumaliza taratibu za kisheria.

Aidha, ameongeza kuwa changamoto nyingine inahusu Hisa za Zanzibar kwa iliyokuwa bodi ya safari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Pamoja na Mapendekezo ya tume ya Pamoja ya fedha.

Hata hivyo, Mkutano huo wa waandishi wa habari umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Ofisi hizo.

Wawekezaji kutoka Misri watua nchini, waahidi kujenga kiwanda kikubwa
Video: 'Kama unaishi kwa sababu ya filamu lazima upige kelele' - JB