Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba, amewataka vijana kuleta mabadiliko chanya katika nchi maaana Vijana ndiyo tegemeo la Taifa.

Ameyasema hayo  leo mjini Unguja alipokua akizindua Baraza la Vijana la Wilaya ya Magharibi A, Makamba amewasisitiza vijana kutumia baraza hilo kama tanuru la kutengeneza mbinu za uongozi na daraja la kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ambao utawafanyana kutokuwa tegemezi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi A, Mwinyiusi Hassan amewataka vijana kuwa nguvu kazi ya Taifa na pia wahakikishe wanalinda na kuheshimu na kuulinda utamaduni wa Nchi yetu.

Makonda atoa agizo kwa watendaji wa kata
Mpina aipongeza singida kwa usafi