Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amewataka Wananchi wa Zanzibar  kuulinda na kuuheshimu Muungano pamoja na mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Ameyasema hayo leo alipokua ziarani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, Makamba amesema kuwa anaipongeza Serikali ya Mkoa kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha  wanasimamia usalama kwa raia wote .

Kwa upande wake, Katibu tawala wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mohamed Ali alitaja changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na uchakavu wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  hivyo kuomba Waziri awasaidie.

Audio: JPM ajibu kero ya wananchi Ubungo kupitia simu ya Makonda 'live'
Audio: Tetemesha yamtambulisha Coyo na ngoma kali ‘Njoo Baadae’