Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, January Makamba amezua gumzo kwenye mtandao wa Twitter baada ya kutoa ushauri wake kwa watumiaji wa lifti za majengo marefu.

Waziri Makamba ambaye ni mtumiaji maarufu na mkongwe pia wa mtandao wa Twitter, ameweka ushauri wake mapema leo kutokana na uzoefu aliokutana nao kwenye huduma za lifti za majengo marefu nchini, unaotokana na watumiaji kuwa na tabia zisizoridhisha.

Kupitia akaunti yake yenye wafuasi zaidi ya 517,000, Makamba alianza kwa kutoa ushauri wa sentensi nne kwenye mazingira manne tofauti, lakini kutokana na maswali ya wafuasi wake, aliongeza tena mazingira mengine kisha wafuasi hao nao kuja na mengine ambayo yalikuwa ya ucheshi pia.

 “Kuna upungufu mkubwa wa ustaarabu kwenye lifti za majengo. Mchango wangu:-1. Mlango ukifunguka, ngoja wanaotoka waishe kabla ya kuingia. 2. Kama kuna mtu mnajuana msianze mazungumzo kwa sauti kubwa. 3. Usitafune BigG kwa sauti 4. Kama tumbo limeharibika, jitahidi usiachie upepo”.

Hata hivyo, mada hiyo iliwakuna wengi huku wengine wakimtaka kutumia mabasi ya mwendo kasi pia ili aone kanuni hizo zinavyoweza kufanya kazi pia kule.

Baada ya kufikisha kanuni au masharti 16, alitoa ruhusa kwa wafuasi wake kuongeza kanuni nyingine. Na huenda leo, hii ikawa tweet iliyozua mjadala mrefu zaidi nchini endapo mwendo wa maoni ya watumiaji wa lifti na magari ya mwendokasi utaendelea.

 

Mwanamke akutwa ndani ya tumbo la Chatu
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine