Makamishna watatu wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) akiwemo Naibu Mwenyekiti wamejiuzulu kwa madai ya kutokuwa na imani na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Wafula Chebukati.

Makamishna hao wamesema kuwa bodi hiyo imeshindwa kutimiza wajibu wake na imeingiliwa na watu wengine katika kutoa maamuzi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi, makamishna hao Consolata Nkatha, Paul Kurgat na Margaret Mwachanya wamesema kuwa Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ameshindwa kuiongoza tume hiyo na kudai kuwa tume hiyo imeingiliwa na watu kutoka nje wanaoshawishi jinsi ya utendaji kazi.

“Kwa muda mrefu sasa, mwenyekiti ameshindwa kutoa muongozo wa utaratibu wa utendaji kazi, kumekuwepo na hali ya kutuhumiana pasipo sababu za msingi,”wamesema maafisa hao

Hata hivyo, Mwenyekiti wa tume hiyo ya IEBC – Wafula Chebukati amesema kuwa hana tarifa zozote kuhusu maafisa hao kujiuzulu zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari.

 

Wataalamu wa silaha za sumu wanyimwa kibali cha kuingia Douma
Marekani kufanya mazungumzo na Japan