Mkuu wa Dawati la Makampuni Binafsi ya Ulinzi na Polisi Wasaidizi Tanzani ACP Issack Katamiti amesema Jeshi la Polisi halitasita kuyachukulia hatua kali za Kisheria Makampuni yote ya ulinzi Binafsi yasiyofata sheria kanuni na taratibu zilizowekwa na Jeshi la Polisi ili kukithi vigezo vya Ulinzi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati operesheni maalum kuyakagua na kufuatilia mienendo ya ufanyaji kazi wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni operesheni endelevu ukaguzi nchi nzima.

ACP Katamiti amesema kuwa endapo watabaini kuwa kuna makampuni hayafuati sheria, taratibu na kanuni na miongozo inayotakiwa ambayo miongozo inatolewa na Mamlaka za serikali, Jeshi la Polisi halitasita kuyafutia kibali.

“Inawezekana kabisa yapo makampuni ambayo hayafuati utaratibu uliopo ikiwemo kutokulipa kodi (TRA), mikataba kwa wafanya kazi inasuasua, wafanyakazi hawapati huduma ya NSSF, na hata wafanyakazi wengine hawana unadhifu katika mavazi yao” amesema ACP Katamiti

Mratibu wa Mfumo wa Kusimamia Sekta Binafsi ya Ulinzi Tanzania (PSGP), Macmillan George amesema kuwa mfumo wa PSGP ni wenye lengo la kusajili wafanyakazi wote waliopo katika katika sekta ya ulinzi binafsi nchini.

”Usajili wa makampuni binafsi, serikali itajua ukubwa ajira kwa kampuni za ulinzi binafsi, lakini pia kuangalia ukubwa huu wa ajira unaendana na mapato ambayo makampuni yanachangia pato la Taifa” amesema Macmillan

”Mfumo huu unasaidia wenye makampuni kumaliza changamoto waliyokuwa wakikutana nayo kuajiri mfanyakazi anafanya uhalifu halafu anahamia kampuni nyingine nako anafanya mengine, kwa usajili huu wa PSGP kila anayesajiliwa atapewa namba ya utambulisho ambayo itakuwa inamtambulisha katika hii sekta na kila atakapo kwenda”

‘Usajili wa makampuni binafsi, serikali itajua ukubwa ajira kwa kampuni za ulinzi binafsi, lakini pia kuangalia ukubwa huu wa ajira unaendana na mapato ambayo makampuni yanachangia pato la Taifa” amesema Macmillan

Kwa upande wake Meneja msaidizi Mamlaka ya Mapato ( TRA) Dodoma Silver Rutagwelera amezitaka kampuni zote binafsi za ulinzi kutunza kumbukumbu zao zote ili kuweza kutambua kwa urahisi utendaji wao wa kazi

“Tunaangalia makadirio na mapato, uwasilishaji wa return za mwezi au mwaka,mikataba ya malindo na jengo,paylow, mishahara ya wafanyakazi ili kuweza kubaini kama kodi inayokatwa na kuwasilishwa ni sahihi pamoja na mengine yanayoweza kujitokeza” amesema Rutagwelera

Naye, Alice Milanzi kutoka Idara ya Kazi mkoa wa Kazi Temeke amesema kuwa wamekuwa wakiangalia mambo mbalimbali ikiwemo stahiki zao mbalimbali kwa mujibu wa sheria ikiwemo mikataba ya kazi, paylow ili kujiridhisha kama wafanyakazi wanalipwa sawa kulingana na kazi wanayofanya.

Kwa upande wa Hassan Dotto Msimamizi wa uandikaji kutoka mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF), amesema kuwa wamekuwa wakifuatilia mishahara inayolipwa kama inaendana katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na kinachowasilishwa katika mfuko huo kama kipo sahihi.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 13, 2022
Maafisa habari wa serikali watakiwa kutoa elimu ya sensa kwa umma