Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud othman amehimiza Kilimo cha Kisasa kinacholenga kukuza biashara na kuiongezea nchi pato, kupitia Soko la
Utalii.

Othman ameyasema hayo katika eneo la Dole, Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja, na kuongeza kuwa Kilimo hicho kinapaswa kuzingatia ujuzi wa kitaalamu katika kuongeza mazao ya biashara yatakayokidhi Soko la Utalii liliopo nchini.

Ameyataja maeneo hayo, kuwa ni Kilimo cha Viungo, Mboga-mboga, Matunda halisi na Uzalishaji wa Vifaranga, kwa kuzingatia matumizi makubwa ya kemikali, ambacho ni rafiki kwa afya za watumiaji wakiwemo wageni wanaotembelea visiwa vya Unguja na Pemba.

“Hakikisheni mnawatumia vyema wataalamu wa kilimo cha kisasa na kuwashajihisha wakulima kukifanya kilimo kuwa cha bishara zaidi ili kukidhi soko kubwa la biashara ya utalii iliyopo
Zanzibar hivi sasa,” amesisitiza jambo hilo Makamu wa Rais Othman.

Hata hivyo, amesema wakulima wengi hawana ufahamu wa kutosha juu ya kilimo chenye tija na kwamba Wizara ina wajibu wa kuhakikisha mageuzi katika sekta hiyo, yanayohusisha mbinu bora na mikakati ya kutokomeza wadudu waharibifu.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo wa Zanzibar, Shamata Shaame Khamis amesema dhamira ya Serikali kupitia Wizara ni kuhamasisha kilimo kinachozingatia uwekezaji wenye tija, kinacholenga faida kwa wakulima na Taifa.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud othman.

Amesema, mwelekeo huo ni muhimu katika uzalishaji wa bidhaa za kilimo za aina mbalimbali, ili kukidhi mahitaji katika masoko ya Zanzibar, na hasa iwapo wataalamu watawajibika
ipasavyo.

Jeshi lawasilisha mabadiliko tozo na ukaguzi
Kenya: Wasiokubali matokeo waende Mahakamani