Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwalea watoto kwa kuzingatia maadili ya kitanzania pamoja na kuongeza umakini katika
maudhui yanayooneshwa katika televisheni.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na waumini wa Kijiji cha kasumo mkoani Kigoma mara baada ya kushiriki Ibada ya kawaida ya katikati ya wiki katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria
Malkia wa Amani iliopo Kijiji hapo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Ibada ya kawaida ya asubuhi iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Joseph Mashaka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani iliopo Kijiji cha Kasumo mkoani Kigoma hii leo Machi 23, 2023.

Amesema ni wazi kwa sasa kumekuwepo na changamoto ya mmomonyoko wa maadili ikiwemo ndoa za jinsia moja ambapo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla inapaswa kukemea vikali ili kuondokana na
taifa lisilofaa kwa vizazi vya sasa na baadaye.

Halikadhalika Makamu wa Rais amewaasa wananchi wa Kasumo na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kutoa ushirikiano wakati huu ambapo serikali inafanya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika mkoa huo
ambayo ni nyenzo muhimu kwa biashara na urahisi wa kufikia huduma za jamii kama vile hospitali na shule.

Rubani afichua madhaifu ajali ya Ndege
Tanzania yaikumbusha Dunia kusimamia ajenda ya Maji