Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan imekanusha taarifa za zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anataka kujiuzulu nafasi hiyo.

Ofisi hiyo imewataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa ni za uongo na kwamba zimelenga kuzua taharuki kwa wananchi.

“Taarifa hiyo ya uchochezi imelenga kuliweka taifa kwenye taharuki. Mheshimiwa Samia Suluhu yuko bega kwa bega na mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi,” imeeleza taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Imewataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuepuka kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani.

Mbeya City Waanza Mazoezi, Mlawa Nje
Henrikh Mkhitaryan: Sina Uhakika Kama Nitakua Fit