Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amewataka Wakuu wa Wilaya kuwa wepesi na wabunifu katika kutatua migogoro ya ardhi na mipaka, wakulima na wafugaji na ile ya wafugaji, wakulima na hifadhi ikiwemo kuhakikisha hakuna migogoro mipya inayoibuka katika maeneo yao.

Dkt. Mpango ameyasema hayo leo hii leo Machi 13, 2023 wakati akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo katika mji wa Serikali Mtumba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.

Dkt. Mpango pia amewasihi Wakuu hao wa Wilaya kudhibiti uhasama ndani ya jamii au na vyombo vya dola, mauaji na kuwa walinzi wa haki za watu wote hususani wanawake na watoto na kuwataka kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao, kwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango vilivyokusudiwa.

Aidha, pia amewataka Wakuu wa Wilaya kuimarisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa kutoa hamasa kwa wananchi hususani vijana ili wawe mstari wa mbele katika shughuli za uhifadhi ikiwemo kupanda miti na kusimamia mipango miji katika maeneo yao.

Mashushushu Horoya AC washtukiwa Dar
Tanzania kushirikiana na Jumuiya ya Madola migogoro, umasikini