Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri taarifa za wajawazito na afya za watoto katika kila kata. ripoti kila baada ya miezi sita.

Ameyasema hayo jijini Dodoma katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa inayolenga kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga nchini iliyopatiwa jina la ‘Jiongeze! Tuwavushe Salama’

Kampeni hiyo ambayo madhumuni yake ni kuhamasisha viongozi wa serikali, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa maendeleo, watoa huduma za afya, familia na jamii kwa ujumla ili kuchangia katika juhudi za taifa za kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na vifo vya watoto wachanga.

“Naagiza kila Mkuu wa Mkoa, aifanye ajenda ya uzazi iwe ya kudumu katika vikao vya halmshauri kuu za mikoa (RCC) na mfuatilie taarifa zote za wajawazito katika kila kata ziwafikie, naamini halitoshindikana ninachohitaji ni uwajibikaji, ifike wakati jamii kwa pamoja iwajibike katika kuungana na kumpatia mwanamke faraja wakati wa kujifungua na tuachane na kauli kwamba mwanamke atazaa kwa uchungu, hebu tuwapunguzie uchungu huo,”amesema Mama Samia

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya mwaka 2017, zinaonyesha kuwa wanawake milioni 2.2 hubeba ujauzito kila mwaka na asilimia 85 hujifungua salama na asilimia 15 pekee ndio hupata matatizo wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua

 

Sita mbaroni kwa njama za kumuua Rais
Boomply, UMG waingia mkataba wa usambazaji muziki