Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdory Mpango ameagiza Wizara za Viwanda na biashara Bara na Visiwani na TAMISEMI kuangalia namna bora zaidi ya kuwatumia wataalamu wa biashara na viwanda waliopo katika manispaa na halmashauri zote nchini ili kuwasaidia wafanyabihra kujiendesha kwa faida na kuchangia pato la Taifa.

Ameyasema hayo leo Julai 5,2021 wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya 45 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam SabaSaba, ambapo amesema serikali inaendelee kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuviweszesha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kuendelea kuimarika kufanya kazi kwa tija.

Aidha Makamu wa Rais Mpango ametoa wito kwa waendesha viwanda nchini kuongeza uzalishaji wa bidhaa za waraji kama vile sukari, mafuta ya kula , unga wa ngano na nyinginezo lakini kuhakikisha wanaondoa urasimu na kuwezesha biashara na wawekezaji badala ya kukwamishana.

Sambamba na hayo pia amewasisitiza wafanyabiashara wa ndani kukumbuka kuna ushindani mkubwa katika biashara, masoko ya ndani, masoko ya nje na kuwahasa kuzingatia mahitaji ya soko na masharti ya mikataba waliyoingia na wateja wao ikiwa ni pamoja na kuzingatia viwango vya bidhaa, ubora unaotakiwa na kufikisha bidhaa kwa sokoni kwa wakati.

Aidha amewasihi wafanyabiashara kutumia Taasisi za kuweka viwango kama TBS, TMDA ili kujiridhisha na ubora wa bidhaa kutoka Tanzania zinazotakiwa kwenda sokoni.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 5, 2021
Manara: Nitatimiza ahadi yangu Jumatano