Makamu wa Rais wa Nigeria, Yemi Osinbajo aliyepata ajali ya helkopta wikendi iliyopita amewatoa wasiwasi wafuasi wake kuwa yuko salama.

Osinbajo alituma ujumbe wake kupitia akaunti yake ya Twitter akiwashukuru pia wafanyakazi wa ndege hiyo kwa jinsi walivyosaidia kupunguza madhara ya ajali hiyo iliyoanguka katikati ya mji wa Kabba.

Mwanasiasa huyo alikuwa katika safari yake kuelekea kwenye mikutano ya kampeni, ambapo yeye na Rais Muhammadu Buhari wanatafuta ridhaa ya kuongoza kwa muhula wa pili, kupitia uchaguzi mkuu utakaofanyika Februari 16 mwaka huu.

Kwa mujibu wa BBC, vyombo vya ulinzi na usalama vimesema kuwa vimeanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo mara moja.

Kampuni ya Caverton Helicopters inayomiliki ndege hiyo imesema watu wote kumi na wawili waliokuwa ndani ya ndege hiyo hawakuumia. Kampuni hiyo imeongeza kuwa chanzo cha ajali ni hali mbaya ya hewa.

Wauguzi wagoma, huduma hospitalini zazorota
Wapinzani kung’ang’ana na sakata la Sh. 1.5 trilioni majimboni