Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewapa Wakuu wa Mikoa ya Geita, Arusha na Kagera pamoja na Wakuu wa Wilaya za mikoa hiyo,  ukomo wa siku wa kutimiza agizo lake linalolenga kuondoa migogoro kati ya Tanapa na wafugaji.

Akizungumza jana jijini Arusha  alipokuwa akikabidhi hundi ya thamani ya shilingi bilioni moja kwa wakuu wa Mikoa 19 inayozunguka hifadhi ya taifa kwa ajili ya kununua madawati, Mama Samia aliwaagiza Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanakamilisha kazi ya kuondoa mifugo inayotoka nje ya nchi pamoja na wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi ya taifa ifikapo Juni 30 mwaka huu.

Aidha, aliwataka Wakuu hao wa Mikoa kuhakikisha ifikapo tarehe hiyo, wawe wameshatenga maeneo maalum kwa ajili ya mifugo ya wananchi wanaoondolewa kwenye eneo la hifadhi ya taifa ili kuondoa migogoro.

Alisema kuwa anafahamu kuwa Mkoa wa Kagera una ng’ombe milioni mbili wanaotoka nje ya nchi na mikoa ya Arusha na Geita kwa pamoja ina ng’ombe milioni tatu kutoka nje ya nchi.

Mama Samia alisisitiza kuwa Mkuu wa Mkoa atakayeenda kinyume na agizo lake ndani ya kipindi kilichotajwa atawajibishwa.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema kuwa Tanapa inatambua mchango wa elimu nchini ndio sababau wameamua kutoa msaada huo wa madawati kwa mikoa 19 inayopakana na hifadhi ya taifa.

Kutokana na msaada huo wa Tanapa, kila wilaya katika mikoa hiyo itapata madawati 300 na kuwaondoa sakafuni wanafunzi 49,500.

 

Mjane aliyemlilia Rais Magufuli akabidhiwa nyumba, Shamba
SERIKALI YATAKIWA KUBOREESHA BAADHI YA MAPUNGUFU KWENYE MWENDOKASI