Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kunahitajika sera na mikakati itakayosaidia kutekelezwa kwa sera za mazingira nchini.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Hali ya Mazingira nchini iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na Benki ya Dunia.

Tunahitaji mipango ya uwekezaji inayotengwa kuelekea kukabiliana na sababu za msingi za changamoto za mazingira,alisema Makamu wa Rais

Aidha, ripoti hiyo imegusia mambo mbalimbali ambayo yanaathiri mazingira nchini, yakiwemo uchafuzi wa hali ya hewa, maji, ukataji miti hovyo lakini pia maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kuwa uharibifu wa mazingira unasababisha vifo vingi vya kimya kimya kuliko vifo vinavyosababishwa na kitu kingine chochote.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird amesema kuwa benki ya Dunia imekuwa mstari wa mbele katika kutafuta majawabu yatakayoweza kuisaidia jamii.

Video: Lazima tujijengee tabia ya kupenda kulipa kodi- Wakili Manyama
Sakata la Mdude Chadema, Msigwa kuhojiwa polisi

Comments

comments