Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Equinor ya Norway, Bi. Nina Koch ametembelea eneo utakapojengwa mradi huo wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG) mkoani Lindi, na kuipongeza Serikali kuchagua eneo la ujenzi wa mradi karibu na kiwanja cha ndege.

Bi. Koch, ametembelea eneo hilo ikiwa ni moja ya muendelezo wa ziara yake ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nishati Januari Makamba na kusema ujenzi katika eneo hilo utarahisisha usafiri wa wafanyakazi na vifaa mbalimbali wakati wa ujenzi na uendeshaji wa mradi.

Waziri wa Nishati, January Makamba mapema leo hii leo (Desemba 8, 2022), alipokutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Equinor ya Norway, Bi. Nina Koch jijini Dodoma pamoja na ujumbe wao.

Aidha, Bi. Koch pia alitembelea Chuo cha VETA kilichopo Mkoani Lindi, ambapo Kampuni zitakazowekeza katika mradi wa LNG, zimekuwa zikitoa ufadhili wa vifaa vya kujifunzia

Hata hivyo, Bi. Koch amemueleza Waziri Makamba kuwa lengo la Kampuni ya Equinor ni kuendelea na kuvifadhili vyuo mbalimbali hasa vya mikoa ya Lindi na Mtwara, ili kuwajengea uwezo kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika ujenzi ma uendeshaji wa mradi wa huo wenye thamani ya zaidi ya trilioni 70.

Bima yawalipa Marubani waliofariki ajali ya ndege Bukoba
Mtoto wa Rais ahukumiwa miaka 12 jela