Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya kitaifa ya Sikuku ya Wakulima(Nanenane) ambayo yatafanyika Viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu.

Maonyesho hayo yanatarajiwa kufungulia Kedho Agosti 1, 2020 na kudumu hadi Agost 8, 2020 ambapo yatajumisha Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi za kilimo, fedha na ufugaji.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswanga, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, amesema maandalizi ya maonyesho hayo yamekamilika huku wadau wote wa maonesho hayo wakithibitisha kushiriki.

”Kwenye ufunguzi ambao utafanyika kesho mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais, tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kumsikiliza kiongozi wetu lakini pia kufika kwenye maonyesho kwaajili ya kujifunza”amesema DC Kiswanga

Aidha amewataka wananchi wa mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara kufika kufika kwenye maonesho hayo, kujifunza Teknolojia mbalimbali za kilimo.

Mbaloni kwa kunajisi watoto
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 31, 2020