Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Hassan Suluhu amezindua rasmi leo kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea inayoendeshwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya mwembeyanga jijini Dar es salaam.

Awali wakati akitoa maelezo ya kuhusu kampeni hiyo Mkurugenzi mkuu wa Takukuru Bw. Valentino Mlowola amesema kwamba kuzindua kampeni ya longa nasi lengo ni kuamsha ari ya wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa ambayo imekuwa kikwazo cha maendeleo hapa nchini.

Kilowola

Bw. Mlowola ameeleza kuwa kampeni ya longa nasi itazunguka nchi nzima kutoa elimu na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kutoa taarifa za rushwa na kuongeza kwamba elimu itatolewa kupitia gari la , makala, vipeperushi , mikutano na kwa njia ya simu kwa kupiga namba ya dharura 113.

Pia katika sherehe za uzinduzi wa kampeni hiyo viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwepo Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejiment ya utumishi na utawala bora Bi.Angela Kairuki ambapo ameipongeza TAKUKURU kwa mapambano dhidi ya wala rushwa na kusema kwamba taasisi hiyo inatakiwa kufanya kazi kwa kutenda haki na kuhakikisha wenye makosa wanashughulikiwa.

Kairuki

Aidha Bi. Kariuki amesisitiza kwamba wananchi wanatakiwa watoe taarifa ili kusaidia kampeni hiyo kufika mbali na kuongeza kwamba juhudi za serikali kupambana na rushwa bado zinaendele na kwamba mahakama maalum ya kupambana na mafisadi inakamilika hivyo punde tuu itaanza kufanya kazi.

Hata hivyo wakati akitoa maneno ya uzinduzi Mh Suluhu ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kutoa taarifa za rushwa katika maeneo yanayowazuunguka ili kutengeneza serikali imara na isiyo omba omba.

Samia-Suluhu

Hata hivyo Bi. Samia amesisitiza kuwa kampeni ya longa nasi inatakiwa kushughulikia taarifa zitolewazo ,kumshukuru na kumjibu mtoa habari na pia wananchi watoe taarifa za kweli pasipo kuingiza chuki au kulipiziana kisasi.

Pamoja na hayo Makamu wa Rais Bi. Samia ameleza kuwa tatizo la sukari nchini linatatuliwa na hali yake itakuwa kama inavyotakiwa kwani wahujumu na mafisadi walioficha sukari wanaendelea kushughulikiwa.

TANZANIA KUIUZIA UMEME ZAMBIA
Mwali Wa ASFC Kukabidhiwa Kwa Mwenyewe Kesho

Comments

comments