Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence jana alikwepa kukutana na kiongozi wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini, Kim Yong-Nam.

Pence alitakiwa kukutana uso kwa uso na kiongozi huyo lakini walijikuta wakikwepa kukutanisha nyuso zao kwenye meza iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya viongozi mbalimbali.

Baada ya Pence kutoonekana katika meza hiyo, Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in alishikana mikono na dada wa kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un aitwaye Kim Yo-jong kwenye ufunguzi wa mashindano ya Olimpics nchini humo.

Matukio hayo yamefanyika wakati ambapo kuna taharuki ya kijeshi kati ya mataifa hayo pamoja na Marekani.

Marekani ambayo ni washirika wa Korea Kusini wanapinga hatua za majaribio ya makombora ya nyuklia inayofanywa na Korea Kaskazini.

Miguna adai atamng'oa Kenyatta madarakani
Video: Wabunge waogopa kukutwa ya Lissu, Watumishi wa umma kicheko

Comments

comments