Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris anatarajiwa kuwasili nchini majira ya saa nne usiku wa Machi 29, 2023 akitokea nchini Ghana ambapo Watanzania wanatarajia kutumia ujio huo kujipatia fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo biashara.

Kamala atakuwa nchini kwa ziara ya kikazi kwa siku tatu, ambapo pia anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hapo kesho Machi 30, 2023.

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris. Picha ya NPR.

Harris ambaye amekuwa nchini Ghana tangu Machi 26, 2023 pia anatarajia kuelekea kituo chake cha mwisho cha ziara yane nchini Zambia, atakapokuwa kwa siku mbili za Machi 28 – April Mosi, 2023.

Akiwa nchini Ghana, Kamala Harris alimsifu Rais wa Taifa hilo Nana Akufo-Addo kwa kanuni zake za kidemokrasia, wakati wa ziara yake na kiongozi huyo wa Afrika Magharibi, ambaye anakabiliwa na tatizo la kumaliza mfumuko wa bei na wasiwasi mpya kuhusu usalama wa kikanda.

Deni la Serikali lafikia Trilioni 71.31
Mbunge Waitara amwaga chozi hadharani, adai ametengwa