Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu amesema wakati serikali na Jamii ya kitanzania inaendelea kupambana na ugonjwa wa Corona lazima jamii iendelee kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mengine ya hatarishi ukiwemo ugonjwa wa Ukimwi.

Ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa anazindua uwekaji wa makasha ya kusambazia kondomu maeneo ya watu na yenye mikusanyiko huku akifafanua takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka takribani watu 72 elfu wanaambukizwa maambukizi mapya ya ukimwi.

Aidha Waziri Ummy ameihasa jamii kuacha dhana potofu ya kumuona tu aliyebeba kondomu kumuhisi kuwa ni muhuni bali jamii ijifunze kujilinda na maambukizi yatokanayo na ngono zembe ambazo zimekua zikiharibu maisha ya baadhi ya watu.

Sambamba na hilo pia amewaagiza watendaji wa TAMISEMI kwa kushirikiana na Shirika la Vijana Tanzania (TAYOA) kuhakikisha wanasambaza makasha hayo na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI hadi maeneo ya Vijijini ambapo baadhi ya jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huo.

Makasha hayo tayari yamefika kwenye halmashauri 169 kati ya halmashauri 184 kwa Tanzania bara hivyo wajitahidi kufikisha maeneo mengi zaidi kuokoa taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Tayoa Peter Masika akimfafanulia jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu namna makasha ya kusambazia kondom yanavyofanyakazi, wakati wa uzinduzi wa makasha hayo jijini Dodoma.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu akiwasili kwenye uzinduzi wa makasha ya kondom mjini Dodoma . Kulia kabisa Mkurugenzi Mkuu wa Tayoa, Peter Masika ambaye amesema wanatarajia kusambaza makasha 80,000 nchini. Mwingine ni Mbunge wa Dodoma Mjini Antony Mavunde
Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu akionyesha kondom aina ya safari mara baaa ya kuitoa kwenye mashine ya kuuzia kondom kwa bei nafuu wakati wa uzinduzi wa makasha ya kondom mjini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tayoa, Peter Masika ambaye amesema wanatarajia kusambaza makasha 80,000 nchini.

Ndumbaro asisitiza matumizi ya Nishati mbadala
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 31, 2021