Kocha Mkuu wa Mbeya Kwanza FC Mbwana Makata ameipigia Magoti Bodi ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’ pamja na Shirikisho la soka nchini ‘TFF’, kufuatia adhabu ya kufungiwa miaka mitano iliyotangazwa na Kamati ya saa 72 juma lililopita.

Makata pamoja na Meneja wa Mbeya Kwanza FC David Naftari walikumbwa na adhabu hiyo, baada ya timu yao kugomea kucheza dhidi ya Namungo FC katika dimba la Ilulu Mkoani Lindi mwanzoni mwa mwezi Mei, kwa madai ya kutokuwepo gari la kubebea wagonjwa (Ambulance).

Kocha huyo mzawa amesema hana budi kuomba radhi kwa kitendo alichokifanya, na amekubalia kuwa mfano kwa wengine ambao wamedhamiria kwenda kinyume na kanuni za soka la Tanzania.

“Natumia fursa hii kuwaomba radhi TFF, Bodi ya Ligi, wadhamini wetu NBC na Azam Media, kuomba radhi kwa kile kilichopelekea kufungiwa miaka mitano”

“Tangu nilipokua nacheza soka hadi sasa nimekua Kocha sijapata onyo lolote ikiwa kuonyshwa kadi ya njano au nyekundu ama kufungiwa, kwa hiyo tunaahidi kuwa mfano mzuri kwa jamii na famnilia ya soka endapo tutafungulia ama kusamehewa.” amesema Kocha Mbwana Makata

Naye David Naftari amesisitiza kuomba msamaha kwa Bodi ya Ligi ‘TPLB’ na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ kwa kosa alilolifanya, na amekiri kujutia kosa hilo na ndio maana amejitokeza hadharani.

“Tunajutia kwa kosa tulilifanya, limetuharibia sana maisha yetu ya soka, kila mmoja anayehusika na soka la Tanzania tunamtaka radhi.” amesema Naftari

Morogoro: Gari yagonga tren mmoja afariki mwingine ajeruhiwa
Franco Pablo: Tuna kazi kubwa ya kufanya Jumamosi