Spika mstaafu wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, Anna Makinda ameiomba Serikali na mamlaka husika kuanza mchakato kusukuma mabadiliko ya Sheria ya Ndoa ili kupanua wigo wa haki za wanawake na watoto nchini.

Ameyasema hayo katika kongamano la kitaifa la haki za Wanawake,lililoandaliwa na Mfuko wa Msaada wa Kisheria Tanzania( LSF) jijini Dar es salaam, Makinda alisema Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 imepitwa na wakati na inahitaji marekebisho makubwa ili kutoa  kwa wanawake nchini.

Makinda alisema marekebisho hayo makubwa au kuandikwa upya hiyo itakuwa  hatua moja kubwa katika kulinda haki za wanawake za kumiliki mali kama vile mashamba na mambo mengine.

Sirro atangaza kiama kwa vibaka na wahalifu Dar
Majaliwa azitaka halmashauri kuanzisha mashamba miti