Watu zaidi ya 10 wanaripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa Ukraine baada ya makombora kirindima usiku kucha kuamkia siku ya Jumatatu na kushambulia vituo vya kijeshi na kituo cha kutolea huduma ya matairi ya gari katika mji wa magharibi mwa Ukraine wa Lyv, gavana wa eneo hilo, Maksym Kozytsky amethibitisha. 

Katika Mji mwingine wa Kreminna, raia wanne wameuawa kwa kupigwa risasi na mmoja kujeruhiwa walipokuwa wakijaribu kuukimbia mji huo, kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Luhansk Serhiy Haidai.

Haidai alionya watu katika taarifa akisema: “Usitoke mafichoni. Usijaribu kuondoka Kreminna peke yako! Ni hatari!” 

Alisema Warusi “walimechukua udhibiti” wa mji huo na mapigano yanaendelea, akiongeza kuwa “kuwahamisha watu kutoka mji huo hauwezekani tena”.

Kwa upande wake naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk alisema: Hakutakuwa na njia ya kuwaondoa raia katika maeneo yaliyoathiriwa kwa siku ya pili mfululizo baada ya maafisa wa Ukraine kushindwa kukubaliana kuhusu njia za kibinadamu.

Vyombo vya habari vya serikali ya Urusi vinaripoti kuwa jeshi lake lilishambulia jumla ya malengo 315 nchini Ukraine usiku kucha na miji kadhaa alisema jeshi la Urusi liliwafyatulia risasi raia waliokuwa wakijaribu kuondoka kwa gari wao wenyewe.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov alisema kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi iliwaangusha wapiganaji wawili wa Ukraine.

“Makombora ya anga ya juu yaliharibu vituo 16 vya kijeshi vya Ukraine usiku wa kuamkia leo,” Aliongeza

Hata hivyo Yuri Sak mmoja wa washauri wa waziri wa ulinzi wa Ukraine, ambaye yuko magharibi mwa Ukraine – amekuwa akizungumza na shirika la habari la BBC kuhusu mashambulio katika mji wa Lviv. 

“Kilichotokea leo ni kitu cha kutisha kwa sababu hili ni shambulio kubwa la kombora [dhidi] ya miundombinu ya kiraia,” aliambia kipindi cha Leo cha BBC Radio 4. 

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Anga ya Magharibi, makombora manne yalipiga Lviv, na kuacha vifaa vikiwa vimeharibiwa vibaya, na moto uliozuka kutokana na mapigo hayo bado unaendelea kuzimwa.

Taarifa zilizotolewa na Maafisa wa Marekani wanaoangazia mzozo huo kati ya Urusi na Ukraine zilisema Urusi imejipanga kwa shambulio la awamu ya pili baada ya mazungumzo ya kila namna ya kusitisha mapigano kugonga mwamba

Simba SC yaiweka kiporo Young Africans
Ahmed Ally arudisha shukurani kwa Mashabiki Simba SC