Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa ahadi ya mifuko 1000 ya cement na magodoro 400 ikiwa na jumla ya thamani ya shil. Mil.44 kwaajili ya ujenzi wa bweni la wasichana,kwa shule ya Sekondari Saint Joseph millenium.

Makonda amesema hayo leo Oktoba 22, 2016  wakati akitoa hotuba katika mahafali ya kidato cha Nne ya shule ya Sekondari, Saint Joseph Millenium iliyopo Goba jijini Dar es salaam alipokuwa amealikwa kuwa mgeni rasmi.

Aidha, ameongeza kuwa wanafunzi kuanzia wa kwanza hadi wa tatu, watakaofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwenye  mtihani wa kidato cha Nne  Mkoa wa Dar es salaam atawasomesha na watakuwa huru  kuchagua shule zozote watakazo taka kwenda kusoma hapa nchini, ameongeza kuwa hata wale watakao faulu vizuri kidato cha sita atawapa zawadi ya shil. Mil.2 kila mmoja.

Hata hivyo ameongeza kuwa kwa upande wa waalimu wanaofundisha masomo ya sayansi ambao watafaulisha vizuri wanafunzi wao watapatiwa zawadi ya shil. Mil.2 na kuwapeleka  mbugani kwaajili ya mapumziko,

Kwa upande mwingine Makonda amewasihi wazazi kutowachagulia watoto masomo ya kusoma ili kuondoa mfumo mbaya ambao umelisababishia  taifa kuwa na wataalamu wasio na sifa na wanaofanya kazi kwaajili ya mshahara, ’’ kumpa mtoto nafasi ya kujichagulia kusoma anachopenda ni kumpa fursa  ya kumwezesha kuwa mbunifu zaidi,’’Alisema Makonda

Sauti Sol yaitoa kimasomaso Afrika Mashariki MTV MAMA, orodha Kamili
Video: Taifa letu limepoteza ubunifu - RC Makonda